.

.

Samatta kaanza mechi za play offs Ubelgiji kwa kufunga katika ushindi wa 4-0

Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena jana Jumamosi ya April 1 2017 kwa KRC Genkinayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kuikaribisha Lokeren katika mchezo wao wa kwanza wa play offs wa Kundi B wa Ligi Kuu Ubelgiji.
Mbwana Samatta ambaye alikuwa katika kikosi cha kwanza cha KRC Genk kilichocheza dhidi ya Lokeren alifanikiwa kuisaidia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa goli 4-0,Mbwana Samatta akifunga goli la pili dakika ya 72.
Goli la kwanza la Genk lilifungwa na Pozuelo dakika ya 45, goli la tatu lilifungwa na Boetiusdakika ya 77 la mwisho lilifungwa na Jose Naranjo aliyeingia dakika ya 84 akitokea benchi na kufunga goli dakika ya 90, ushindi huo umeifanya KRC Genk kuongoza Kundi B lenye timu sita kwa kuwa na magoli mengi.

Magazeti ya Tanzania March 31, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo


















Taarifa kuhusu stori za nyasi bandia za Simba kupigwa mnada na TRA


Moja kati ya stori kubwa iliyokuwa ikijadiliwa kwa wapenda soka bongo jana ni kuhusiana na habari za nyasi bandia za timu ya Simba kuandikwa kuwa zitapigwa mnada na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutokana na kushindwa kuzilipia kodi bandarini, Simba waliomba msamaha wa kodi lakini imeshindikana.

Lakini kuna taarifa pia zilizotolewa baadae kuwa mtanzania Mbwana Samatta aliyewahi kucheza Simba ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji amezilipia kodi hizo, ukweli kutoka katika ukurasa rasmi wa msemaji wa Simba Haji Manara na TRA ni kuwa Samatta hajalipia kodi ya nyasi hizo.

Ukweli wa taarifa rasmi ni kuwa Simba wameongezewa muda wa siku 14 wazilipie kodi nyasi zao hizo bandia ambazo wanampango wa kuziweka katika uwanja wao wa mazoezi wa Bunju, katika siku 14 walizopewa Simba tayari zimebakia siku tatu pekee

PATA HABARI ZA KWENYE KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA KWENYE MAGAZETI YA LEO 29.3.2017,UDAKU, SIASA NA MICHEZO




MATOKEO YA STARS NA BURUNDI LEO

Taifa stars imewaadhibu BURUNDI Kwa jumla ya magoli 2 - 1
magoli ya stars yakiwekwa kambani na Simon Msuva pamoja na Mbaraka Yusufu wakati goli pekee la  burundi likiwekwa kambani na mchezaji wa klabu ya Simba sc Laudit Mavugo. Mpaka dakika ya mwisho Stars 2 na BURUNDI 1.

STARS vs AMAVUBI (BURUNDI) LEO JIONI NDANI YA AZAM TV ...MAVUGO NDANI

Image result for taifa stars


Taifa Stars ya Tanzania leo Machi 28, 2017 saa 10:00 jioni inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.

Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.
Tayari Intamba Murugamba wametua nchini tangu juzi Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko, Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini. jana Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ndani ya kikosi hicho wamo washambuliaji wawili wanaotamba katika klabu za Simba na Young African za Dar es Salaam. Nyota hao ni Amisi Tambwe wa Young Africans na Laudit Mavugo wa Simba.
Jana Jumatatu Machi 27, 2017 saa 8.30 alasiri nyota hao wakiongozana na kocha wao watazungumza na wanahabari namna walivyoajiandaa kucheza na Taifa Stars ambayo pia ina nyota wengi wanaocheza na wachezaji hao wa Burundi katika klabu za Simba na Young Africans.
Wakati Mavugo ni mshambuluaji, anatarajiwa kuwa na wakati mgumu mbele ya walinzi mahiri ambao pia wako Simba kama vile Abdi Banda na Mohammed Hussein wakati Andrew Vicent anayetoka Young African atakuwa kisiki kwa Tambwe wanayecheza naye timu moja kama makocha watawapanga.
Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.
Katika kuunga mkono wito wa Kocha Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio kitakuwa ni Sh 3,000.
Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh 10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.