.

.

Magazeti ya Tanzania March 31, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo


















Taarifa kuhusu stori za nyasi bandia za Simba kupigwa mnada na TRA


Moja kati ya stori kubwa iliyokuwa ikijadiliwa kwa wapenda soka bongo jana ni kuhusiana na habari za nyasi bandia za timu ya Simba kuandikwa kuwa zitapigwa mnada na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutokana na kushindwa kuzilipia kodi bandarini, Simba waliomba msamaha wa kodi lakini imeshindikana.

Lakini kuna taarifa pia zilizotolewa baadae kuwa mtanzania Mbwana Samatta aliyewahi kucheza Simba ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji amezilipia kodi hizo, ukweli kutoka katika ukurasa rasmi wa msemaji wa Simba Haji Manara na TRA ni kuwa Samatta hajalipia kodi ya nyasi hizo.

Ukweli wa taarifa rasmi ni kuwa Simba wameongezewa muda wa siku 14 wazilipie kodi nyasi zao hizo bandia ambazo wanampango wa kuziweka katika uwanja wao wa mazoezi wa Bunju, katika siku 14 walizopewa Simba tayari zimebakia siku tatu pekee

PATA HABARI ZA KWENYE KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA KWENYE MAGAZETI YA LEO 29.3.2017,UDAKU, SIASA NA MICHEZO




MATOKEO YA STARS NA BURUNDI LEO

Taifa stars imewaadhibu BURUNDI Kwa jumla ya magoli 2 - 1
magoli ya stars yakiwekwa kambani na Simon Msuva pamoja na Mbaraka Yusufu wakati goli pekee la  burundi likiwekwa kambani na mchezaji wa klabu ya Simba sc Laudit Mavugo. Mpaka dakika ya mwisho Stars 2 na BURUNDI 1.

STARS vs AMAVUBI (BURUNDI) LEO JIONI NDANI YA AZAM TV ...MAVUGO NDANI

Image result for taifa stars


Taifa Stars ya Tanzania leo Machi 28, 2017 saa 10:00 jioni inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.

Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.
Tayari Intamba Murugamba wametua nchini tangu juzi Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko, Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini. jana Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ndani ya kikosi hicho wamo washambuliaji wawili wanaotamba katika klabu za Simba na Young African za Dar es Salaam. Nyota hao ni Amisi Tambwe wa Young Africans na Laudit Mavugo wa Simba.
Jana Jumatatu Machi 27, 2017 saa 8.30 alasiri nyota hao wakiongozana na kocha wao watazungumza na wanahabari namna walivyoajiandaa kucheza na Taifa Stars ambayo pia ina nyota wengi wanaocheza na wachezaji hao wa Burundi katika klabu za Simba na Young Africans.
Wakati Mavugo ni mshambuluaji, anatarajiwa kuwa na wakati mgumu mbele ya walinzi mahiri ambao pia wako Simba kama vile Abdi Banda na Mohammed Hussein wakati Andrew Vicent anayetoka Young African atakuwa kisiki kwa Tambwe wanayecheza naye timu moja kama makocha watawapanga.
Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.
Katika kuunga mkono wito wa Kocha Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio kitakuwa ni Sh 3,000.
Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh 10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.

MAZOEZI YANAENDELEA HAPA HANDENI SEKONDARI

Chini ya HUSSENI SAKIBWANA, Mazoezi ya anaendelea , muda huu timu ya kurugenzi  Fc ikijifua kwa hali na Mali.. Karibu ni wadau wote.




ZOEZI LEO SAA KUMI NA NUSU JIONI. UWANJA NI HANDENI SEKONDARI



Wadau wote wa timu ya mpira ya KURUGENZI FC HANDENI. mnaombwa kufika mapema uwanjani kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya mechi ijayo siku ya jumamosi asubuhi na timu ya WATUMISHI MISIMA.
njoo mapema ili tufanye zoezi kwa pamoja. Njoo kwa wingi  upate nafasi ya kutokea kwenye blog yetu

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA BLOG YA HANDENI KURUGENZI FURSA

 Hapa wadau wakubwa wa handeni kurugenzi FC wakiwa katika mjadala mfupi wa uzinduzi wa blog hii ya HANDENI KURUGENZI FC, utakao fanyika siku ya Jumamosi  1/4/2017 kwenye uwanja wa handeni sekondari . Vinywaji na nyama choma ndani ya nyumba.
ubishani wa kuhusu ipi iwe timu mualikwa , ambapo timu ya mpira wa miguu ya MISIMA WATUMISHI ilipata kura nyingi na hivyo ikateuliwa kama timu rafika katika uzinduzi huo wa HANDENI KURUGENZI FC FURSA BLOG.
 Vinywaji vilikuwepo pia, kutoka kushoto ni Bw Mkalimoto,(IT OFFICER KURUGENZI FC) Bw Cirrus (KATIBU NA MSEMAJI WA TIMU) Bw Ngatte (MCHEZAJI NA MSHAURI WA TIMU) na Bw Nnko (MJUMBE NA KATIBU KAMATI YA MAANDALIZI)

NAKUONA NAKUONA............UNAKITU CHA COCA COLA BROOOOOO!!!!!!!!!!!!! CHIEF NNKO

HABARI PICHA YA BONANZA LILILOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI 25/3/2017 SIMBA VS YANGA

Baadhi ya wanachama na wachezaji wa KURUGENZI FC baada ya bonanza la simba na yanga mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2.

Moja ya wadau muhimu katika timu ya KURUGENZI FC kiungo mkabaji bwana Six na kiungo mshambuliaji Bwana  George chitanda.


kwa umakini mkubwa sana wadau wa Kurugenzi Fc wakifuatilia kikao hapo Jana baada ya bonanza
                       baadhi ya wachezaji wakijiandaa kwa mtanange wa kukata na shoka

 hapa viongozi wakijadili mambo muhimu kabla ya bonanza



KURUGENZI FURSA -HANDENI


Habari waungwana ! baada ya bonanza tulilo fanaya siku ya jana Jumamosi ,kilifanyika kikao cha viongozi na baadhi ya wadau wa soka (KURUGENZI FC) na yafuatayo ni mapendekezo .
1. Kuna ushiriki wa wanakurugenzi kwennye sherehe ya mwenzetu Bwana Mkalimoto anaetarajia kufunga ndoa tarehe 13/5/2017 , kwa maana hiyo tukiwa kama wadau wakubwa na ndugu wakaribu tunaombwa kuchangia tsh 30000/= Mchango uwasilishwe kwa bwana Ernest Ngate, hii ni kwa Ujirani na Udugu Usio wa lazima .tuna ombwa uguswe na Umoja huu.

2. Tumekubaliana kwa pamoja kuisajili timu katika ligi daraja la NNE, pia tumeafikiana kuwasajili baadhi ya vijana ambao watakuwa na kuonyesha morali na timu hii ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa vijana ya kucheza mpira. Kwa pamoja tunaombwa kushirikiana kwa hali na mali kuweza kuipa sapoti TIMU HII YA KURUGENZI FC
     Katika hilo tumekubaliana kuanaza usajili siku ya jumatatu, hapo tutapiga picha (passport size) na kujaza form za usajili .Shukrani kwa Bw Mkalimoto kufadhili gharama za picha  kwa wachezaji hasa wale wanafunzi wasio na uwezo. Na pia Shukrani za kipekee zimwendee Bwana Kimwaga  Ambaye ametuahidi kulipa Tsh 40000 kama Gharama za kuigiza timu kwenye ligi.

3. Pia kubwa zaidi ni wazo la mwenyekiti ambalo lilipata kuungwa mkono na watu wote walio kuwepo kwenye kikao hicho. hii ni kuhusu kuvuka mipaka katika ustawi wa  kurugenzi kama timu na wanakurugenzi kwa ujumla. Ambapo tumependekeza kuwa  na vitege uchumi na msingi wake utakuwa ni michango yetu wenyewe . Kwa sauti moja tumeamua  kuanzia mwezi wa nne tutakuwa na michango ya kila mwezi ikiwa ni kama ADA ya tsh 5000, ya uanachama na lengo letu la kuwa na kurugenzi Fursa. Ambayo itawasilishwa kwa Mweka Hazina wetu Bwana Adili kabla ya tarehe 28 ya kila mwezi na baada ya hapo utapata fursa ya moja kwa moja ya kujiunga na group la handeni KURUGENZI FURSA. Baada ya kupita tarehe 28/4  mwanachama ambaye atakae jiunga atatakiwa kulipa kiingilio na ada ya mwezi.
4. taratibu za mawasiliano zinatarajiwa kutanuka zaidi kwani tutakuwa na blog na website ya kurugenzi Fc ambayo mpaka sasa blog iko hewani kwa anuani ya kurugenzifc.blogspot.com ,YOUTUBE akaunti kwa ajili ya kujitangaza kimataifa zaidi na tanzania kwa ujumla

Mwisho niseme kunafursa nyingi tutazipata ndani ya kurugenzi FC
Wako Cirrus Mahimbi- Katibu na Msemaji wa kurugenzi FC na 
           Mr Mkalimoto- IT OFFICER kurugenzi FC