Habari waungwana ! baada ya bonanza tulilo fanaya siku ya jana Jumamosi ,kilifanyika kikao cha viongozi na baadhi ya wadau wa soka (KURUGENZI FC) na yafuatayo ni mapendekezo .
1. Kuna ushiriki wa wanakurugenzi kwennye sherehe ya mwenzetu Bwana Mkalimoto anaetarajia kufunga ndoa tarehe 13/5/2017 , kwa maana hiyo tukiwa kama wadau wakubwa na ndugu wakaribu tunaombwa kuchangia tsh 30000/= Mchango uwasilishwe kwa bwana Ernest Ngate, hii ni kwa Ujirani na Udugu Usio wa lazima .tuna ombwa uguswe na Umoja huu.
2. Tumekubaliana kwa pamoja kuisajili timu katika ligi daraja la NNE, pia tumeafikiana kuwasajili baadhi ya vijana ambao watakuwa na kuonyesha morali na timu hii ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa vijana ya kucheza mpira. Kwa pamoja tunaombwa kushirikiana kwa hali na mali kuweza kuipa sapoti TIMU HII YA KURUGENZI FC
Katika hilo tumekubaliana kuanaza usajili siku ya jumatatu, hapo tutapiga picha (passport size) na kujaza form za usajili .Shukrani kwa Bw Mkalimoto kufadhili gharama za picha kwa wachezaji hasa wale wanafunzi wasio na uwezo. Na pia Shukrani za kipekee zimwendee Bwana Kimwaga Ambaye ametuahidi kulipa Tsh 40000 kama Gharama za kuigiza timu kwenye ligi.
3. Pia kubwa zaidi ni wazo la mwenyekiti ambalo lilipata kuungwa mkono na watu wote walio kuwepo kwenye kikao hicho. hii ni kuhusu kuvuka mipaka katika ustawi wa kurugenzi kama timu na wanakurugenzi kwa ujumla. Ambapo tumependekeza kuwa na vitege uchumi na msingi wake utakuwa ni michango yetu wenyewe . Kwa sauti moja tumeamua kuanzia mwezi wa nne tutakuwa na michango ya kila mwezi ikiwa ni kama ADA ya tsh 5000, ya uanachama na lengo letu la kuwa na kurugenzi Fursa. Ambayo itawasilishwa kwa Mweka Hazina wetu Bwana Adili kabla ya tarehe 28 ya kila mwezi na baada ya hapo utapata fursa ya moja kwa moja ya kujiunga na group la handeni KURUGENZI FURSA. Baada ya kupita tarehe 28/4 mwanachama ambaye atakae jiunga atatakiwa kulipa kiingilio na ada ya mwezi.
4. taratibu za mawasiliano zinatarajiwa kutanuka zaidi kwani tutakuwa na blog na website ya kurugenzi Fc ambayo mpaka sasa blog iko hewani kwa anuani ya kurugenzifc.blogspot.com ,YOUTUBE akaunti kwa ajili ya kujitangaza kimataifa zaidi na tanzania kwa ujumla
Mwisho niseme kunafursa nyingi tutazipata ndani ya kurugenzi FC
Wako Cirrus Mahimbi- Katibu na Msemaji wa kurugenzi FC na
Mr Mkalimoto- IT OFFICER kurugenzi FC

Salama wana kurugenzi
ReplyDelete